NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

Upelelezi KESI YA VIGOGO WA DART WAFIKIA HAPA


UPELELEZI wa kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5 inayowakabili mabosi watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), akiwemo Mtendaji Mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo, umekamilika.

Wakili wa serikali, kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Stella Mafuru alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakati kesi hiyo ilipotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi.

 Hakimu Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 12 mwaka huu itakapotajwa kwa ajili ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali. Kesi hiyo ilitajwa mbele ya Hakimu Shahidi kwa kuwa, Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage anayesikiliza kesi hiyo, hakuwepo.

Mbali na Asteria, washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo ya uhujumu uchumi ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa mradi huo, Francis Kugesha na Mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.

Inadaiwa kati ya Septemba Mosi na Oktoba Mosi mwaka 2013, Kinondoni Dar es Salaam, Asteria, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 83.5.

Katika mashitaka yanayomkabili Mwakatobe, inadaiwa Juni 29, 2005 katika ofisi za Kodi Ilala, Dar es Salaam, alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA), wakati akiwasilisha taarifa ya fedha ya mwaka 2004 na ya 2005 ya kampuni yake ya Yukan Business, jambo lililosababisha alipe kodi ndogo.

Washtakiwa walikana mashitaka yao kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aliwasilisha hati ya kuruhusu mahakama hiyo, kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

 chanzo>mtembezi 

 

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment