Crystal palace chini ya kocha Alan Pardew watacheza hatua ya nusu fainali kombe la FA. Kwenye ligi kuu ya uingereza wapo nafasi ya 15 huku zikiwa zimebaki mechi 8 msimu wa ligi kumalizika, lakini mwenendo wa crystal palace tangu kuanza kwa mwaka mpya 2016 inatia wasiwasi tena kuna uwezekano wa kumaliza nafasi ya chini zaidi ya hapo.
Baada ya kucheza michezo kumi iliyopita hivi karibuni, Alan Pardew amepata pointi mbili tu. Lakini hadi mwanzoni mwa mwaka mpya Crystal Palace walikuwa wamevuna pointi 31 baada ya mechi 19 za ligi.
Crystal palace haipo mahali salama sana kwenye msimamo wa ligi, kwani tofuati kati yao na timu ambayo ipo nafasi ya 18 Norwich City ni pointi 8. Hivyo Alan Pardew asipokuwa makini kuna uwezekano wa kuporomoka zaidi kwenye msimamo wa ligi au kushuka daraja.
Yawezekana ni ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Crystal Palace hawatengenezi nafasi za kufunga, pia udhaifu wa safu ya ulinzi. Lakini ni kawaida kwa Alan Pardew kufanya vibaya mechi za mwishoni akiwa na vilabu tofauti vya England. Makala hii inakupa rekodi tofauti za Alan Pardew kuhusu kufanya vibaya mechi za mwishoni mwa ligi akiwa na Newcastle United
Newcastle united
- 2013/2014 – alipoteza mechi 7 kati ya 8 za mwisho
- 2012/13 – alishinda mechi 2 kati ya 9 za mwisho
- 2011/12 – alipoteza mechi 3 kati ya 4 za mwisho
- 2010/11 – alishinda mechi 3 kati ya 17 za mwisho
chanzo>shafiidauda.
0 comments:
Post a Comment