NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

JE?UNAJUA INACHOENDELEA KATI YA MOURINHO NA MANCHESTER UNITED?

Kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho imeripotiwa kuwa yuko mbioni kujiunga na klabu ya Manchester United baada ya msimu kuisha na atakuwa kocha ambae atalipwa hela nyingi kuliko makocha wote duniani imeripotiwa na gazeti la Express kuwa paundi milioni 60 ndio thamani ya kocha huyu wa kireno.

Jose Mourinho mara nyingi hatulii sehemu moja kutokana na kutaka matokeo zaidi na mafanikio pasipo kutengeneneza timu inasemekana kocha huyo pindi atuaapo manchester united ana taratibu ya kuja na wachezaji wake ambapo tushawahi kuona timu nyingi alizopitia.

Baada ya kurejea Chelsea aliwaondoa Juan Mata na  Kevin  Debruny  na kuwa  chukua Zuma,Andrie Schurrle pamoja na Roicy Remmy.

Vyombo mbalimbali vya habari vina ripoti kuwa moja ya chaguo lake ni Harry Kane wa Totenhham pamoja na Rafael Verane kutoka Madrid  na kuna wachezaji wataondoka klabuni hapo  kwa ajili ya kuwapisha wachezaji ambao kocha huyo ata wahitaji.

Mashabiki wa Manchester United kwa sasa hawataki mpira mzuri wanataka matokeo kulingana na kauli zao wenyewe wana bariki ujio wa Mourinho kwani wanaamini kuwa ataweza kuleta mapinduzi ya kukosa ubingwa wa EPL na kukosa michuano mikubwa ambapo timu hiyo haijapata matokeo mazuri tangu Alex furgason  astafu mwaka 2012.

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment