NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

RAIS MAGUFULI AWAKUMBUKA WAZEE WALIOATHIRIKA NA UKOMA SIKUKUU YA PASAKA



RAIS  wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania dkt John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya pasaka kwa wazee wasiojiweza  huku wakisumbuliwa na maradhi ya  ugonjwa wa ukoma  nakulelewa  katika Kambi ya Kolandoto iliyopo  manispaa ya Shinyanga.

Zawadi zilizotolewa  ni mbuzi wawili,kilo 100 za mchele na mafuta ya kupikia lita 20  vyote vikiwa na thamani ya shilingi 380,000 kwa ajili ya wazee hao 23 baadhi yao wakiwa ni  wakisumbuliwa na ugonjwa wa ukoma na  pamoja na watoto 13 wanaishi katika kambi hiyo.  



Akikabidhi zawadi hizo jana  kwa niaba ya Rais,katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Abdul Dachi alisema rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ameona ni vyema kusherehekea sikukuu ya pasaka kwa kuwapatia zawadi wazee hao ambao baadhi yao ni wagonjwa wa ukoma.


“Kutokana na mheshimiwa rais kuwa na majukumu mengi amenituma kuwakabidhi zawadi hii ya pasaka mheshimiwa Rais na familia yake anaungana na wazee wa Kolandoto kusherekea sikukuu hii ameomba zawadi hii muipokee”alisema katibu tawala Dachi.

Akipokea zawadi hiyo kwa niaba ya wenzake,mwenyekiti wa kambi hiyo mzee Samora Maganga alimshukuru rais Magufuli kwa kuwakumbuka na kumuomba kuendelea kusaidia wazee katika jamii kwani wanakumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo huduma za matibabu katika vituo vya afya.


“Tunamshukuru  Rais wetu,ameonesha kujali wazee,tunamtakia kila heri katika uongozi wake kwani anaonesha kiasi gani yuko pamoja na watu wananchi wake”,alisema mzee Maganga.


Naye mlezi msaidizi katika kituo hicho cha wazee Evodia Ndaka alisema kituo hicho kinakabiliwa na upungufu wa vyumba vya kulala wazee hao kutokana na baadhi ya majengo kuharibika na kusababisha vyumba vilivyopo kutumiwa na wazee zaidi ya mmoja.


Hata hivyo aliiomba  serikali kuzifanyia ukarabati mkubwa nyumba za makazi hayo ya wazee kutokana na majengo yake kuchakaa hali inayowafanya waishi kwa wasiwasi mkubwa na kwamba wamekuwa  wakilazimika kuzihama wakati wa mvua inaponyesha kutokana na kuvuja huku nyingi kati ya hizo tayari sehemu za kuta zake zimebomoka.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment