Kamati
ya bunge ya huduma za jamii imeitaka Wizara ya Afya ijieleze ndani ya
siku saba kwanini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, aliwasimamisha
watumishi wa Afya wa hospitali ya Butimba bila kufuata hatua stahili.
Mapema
mwezi huu, Magesa Mulongo aliwasimamisha kazi madaktari 3, manesi 6, na
wafanyakazi wengine 2 wa hospitali ya Butimba kwa madai mbalimbali,
yakihusisha kifo cha watoto mapacha. Lakini Mulongo alijitetea maamuzi
yake kuwasimamisha, akisema ilitokana na tendo walilofanya kutoendana na
sheria za kazi.
Mwenyekiti
wa kamati Raphael Chegeni, alisema kamati iligundua kwamba kulikuwa na
matumizi mabaya ya madaraka katika maamuzi ya mkuu wa mkoa. Na kwamba
mkuu wa mkoa hakuomba taarifa ya utenda kazi ili kutambua matatizo ya
hospitali.
Mmoja
wa wanakamati Mhe. Zitto Kabwe ndiye aliuliza ni kitu gani hasa
kilichosababisha mkuu wa mkoa kusimamisha watumishi hao, kwani kuna
wagonjwa wengi wanaofariki katika hospitali husika kwa kukosa tiba na
wengine wakiwa na shida mbalimbali.
Raphael Chegeni alisema mkuu wa mkoa hakufuata kanuni, zinazohitaji watumishi wa afya kusimamishwa na mabaraza yao.
"Kamati
imejiridhisha kwamba mkuu wa mkoa aliwasimamisha wafanyakazi hawa wa
afya kwa kutumia nguvu ya kisiasa" alisema Raphael Chegeni. Pia alionya
wanasiasa, kuchanganya siasa na utoaji wa huduma za afya, hususani
maeneo ya vijijini, kwani mwisho wa siku itawaamiza wakaazi wa vijijini.
Akichangia,
mbunge wa viti maalumu, Mhe. Suzan Lyimo alisema viongozi wa serikali
wanapaswa kutambua mchango wa watumishi wa afya wanaofanya kazi kubwa
kuokoa maisha.
Kamati
pia ilishauri wizara kuboresha mazingira ya kazi ya wafanyakazi wa
afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na marupurupu.
0 comments:
Post a Comment