NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

KASIGA:Serikali itimize sera kwa albinism

Yassini Kasiga katibu wa chama cha watu wenye albinilism mkoa wa Morogoro                         





Serikali imetakiwa kusimami mipango na mikakati waliyoiweka kati sera hasa kwa kundi la watu wenye ulemavu wa ngozo Albinisim

Akizungumza na newspointtz Katibu wa chama cha albinism Tanzania mkua wa Morogoro (TAS) Yassini Kasiga alipokuwa akikabizi vitabu 15 vya albinism katika chuo cha uandishi wa habari Morogoro (MSJ)

Aidha kasiga alisema jamii ya kitanzania inapaswa kubadilika na kupata elimu mbalimbali juu ya watu wenye albinism kwani kuna wimbi kumbwa la mauaji ya watu wenye albism


Hata hivyo alimesema Chama cha Albinism mkoa wa Morogoro (TAS) kinatembelea taasisi mbalimbali ili kuendeleza elimu juu ya watu wenye albinism na kufanya jamii ibadilike na kuachana na dhana potofu ya kuua watu wenye albinilism

“Jamii inapaswa kubalika kwa namna mbalimbali kwani kuua albinism ni jambo la kinyama katika jamii ya kitanzania hivyo tabia hii ikomeshwe katika jamii zetu”alisema kasiga


Pia alisema wameamua kuleta vitabu 15 MSJ kwani ni chuo kinachotoa taaluma ya uandishi wa habari nchini hivyo itafanya jamii kuelimika hasa kwa kuwatumia waandishi wa habari kwani wao hufanya kazi ya kijamii

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment