Halmashauri
ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza Machi 22 kuwa ndiyo kitafanyika
kikao cha Baraza la Madiwani wa Dar es Salaam kujadili ajenda moja ya
uchaguzi wa meya.
Uchaguzi
huo umeahirishwa mara tatu kwa sababu mbalimbali, ikiwamo zuio batili
la mahakama lililowekwa na makada wa CCM, katika Mahakama Hakimu Mkazi
wa Kisutu.
Hata
hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), George Simbachawene
hivi karibuni, alisema zuio hilo ni batili na kuagiza Halmashauri ya
Jiji la Dar es Salaam kufanya uchaguzi huo kabla ya Machi 25.
Kaimu
Mkurugenzi wa jiji hilo, Sarah Yohana alisema jana kuwa uchaguzi huo
utafanyika Machi 22 kuanzia saa 4.00 asubuhi ukumbi wa Karimjee.
Alisema
maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika, ikiwamo kusambaza barua kwa
viongozi wa vyama husika na wajumbe watakaoshiriki kikao hicho
cchanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment