Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Njombe – TACAIDS Abubakari Magege akiongea na washiriki wa kipindi cha redio cha shuga katika uzinduzi rasmi wa msimu mpya wa kipindi hicho kitakachoanza kuruka tena katika redio mbalimbali nchini |
Waratibu wa Shuga
Radio drama series msimu wa pili - Pendo Laizer na David
Sevuri wakichanganua ushiriki wa watangazaji na vikundi vya wasikilizaji |
Mratibu wa Ukimwi kutoka Tume ya Kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa - TACAIDS,Fadhila Mturi akiongea na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina elekezi |
Vipindi vya redio vya
Shuga vitaanza kuunguruma tena
kupitia redio mbalimbali nchini kuanzia wiki ya
pili ya mwezi wa nne mwaka huu. Vipindi hivyo vinalenga kuwaelimisha vijana
kuhusu maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, usawa wa jinsia, kufanya maamuzi
sahihi, matumizi sahihi ya kondomu na kuepukana na msongo rika.
Mfulilizo huu wa mchezo
wa redio wa Shuga unawalenga
zaidi vijana hususan wasichana, kwa kuangalia
mtazamo
wao, matarajio yao, changamoto wanazopitia
ili kutimiza
malengo yao na jinsi wanavyopambana na maisha yao ya kila
siku.
Mchezo wa redio wa
Shuga ulianzishwa mnamo mwaka 2014
kwa ushirikiano kati ya MTV, HIV and AIDS
Free
Generation, Shirika la TACAIDS pamoja na UNICEF. Baada
ya mafanikio
makubwa msimu wa kwanza, TACAIDS na
UNICEF pamoja na wadau wengine waliamua
kupanua wigo
wa program hii kwa kuandaa vipindi zaidi ili kuimarisha
tabia
chanya zilizojengwa katika msimu wa kwanza wa
vipindi vya Shuga.
Katika kuboresha utoaji
elimu kuhusiana na mahudhui ya
vipindi, mashirika ya UNICEF pamoja na TACAIDS
kwa
kushirikiana na kampuni ya True Vision Production
wanaendesha mafunzo elekezi
kwa vituo vya radio za jamii,
mameneja wa radio shiriki, watangazaji na
waandishi wa
habari pamoja na kwa waratibu wa UKIMWI ngazi za
Halmashauri na
Mkoa, ambapo warsha hii inafanyika
mkoani Iringa.
Radio zitakazoshiriki
katika urushaji wa vipindi vya Shuga msimu wa pili ni Clouds FM, Nuru FM –
Iringa, Kitulo FM – Makete, Kyela FM – Kyela pamoja na Furaha FM, Hope FM,
Qibla Ten FM za Iringa
chanzo>Zanziblogg
0 comments:
Post a Comment