Wakati Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, akidai wabunge wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wanakamatwa bila sababu za msingi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, amesema hakuna mtu anayekamatwa bila sababu na kwamba yeyote atakayebainika kufanya kosa, atasweka ndani bila kujali chama chake.
Machi
Mosi, mwaka huu, Mbowe aliwaeleza waandishi wa habari kwamba wabunge na
madiwani kutoka Ukawa, wanadhalilishwa na kunyanyaswa kila kona nchini
na kwamba hizo ni juhudi za kurudisha nyuma maendeleo ya kazi za
viongozi hao.
Hivi
karibuni, Waziri Kitwanga alisema kuwa wananchi watambue kwamba askari
polisi ni rafiki wa raia mwema, hivyo hawawezi kumkamata mtu asiyetenda
kosa.
“Nitamshangaa
askari polisi, mtu anatenda kosa pale wasimkamate eti kwa sababu tu ni
mbunge wa upinzani. Awe wa CCM, awe wa upinzani watakamatwa, mimi
nimeshawaeleza.
“Nimeshawaeleza
wazi kabisa, mimi nitasimamia haki tu, tofauti na hapo hapana, wewe
ungeona yule mama alivyopigwa na wabunge(Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Theresia Mmbando) inaumiza sana. Nilichukia sana lakini hata
sikuwasemesha polisi, nilikaa kimiya tu niwaone watafanyaje.
“Niliamua kuwapima, ‘infact’ (kwa kweli) hawa watu hata dhamana wasingewapa kwa kitendo hicho,” alisema Kitwanga.
0 comments:
Post a Comment