MBUNGE
wa Ubungo, Saed Kubenea amekamatwa na Jeshi la Polisi leo asubuhi
wakati akiwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Kubenea amekamatwa na polisi akituhumiwa kushiriki kumpiga Terresia Mmbando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mmbando
alikuwa mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es
Salaam uliofanyika wiki mbili zilizopita na baadaye kuahirishwa hatua
ambayo iliibua malumbano.
Kubenea alikwenda leo mahakamani kuendelea na kesi yake inayohusu kumtukana Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Kesi
hiyo ilifunguliwa tarehe 15 Desemba mwaka jana baada ya wawili hao
kukutana kwenye Kiwanda cha Nguo cha TOOKU kilichopo Ubungo, jijini Dar
es Salaam.
Katika
tuhuma za kumpiga Mmbando, waliokamatwa katika hatua ya kwanza ni
Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga na madiwani
wawili ambao kwa sasa wapo nje kwa dhamana.
Baada ya kupata dhamana Mdee alisema “Watake wasitake wataachia, hapa ni Ukawa tu. Yote haya yana mwisho lakini wajue kuwa namba ‘zinatufeva’ na si vinginevyo.”
Uchaguzi
wa Meya wa Jiji la Dar s Salaam ndio chanzo cha kukamatwa kwa Kubenea
na wengine waliotangulia ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na vyama
vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) vimekuwa vikisigana.
Ukawa
wanalalamika kuminywa na Halmashauri ya Jiji kwa madai ya kushirikiana
na CCM. Ukawa wameeleza kuwa zinafanyika hujuma ili CCM ishinde Umeya wa
Jiji.
Jumla
ya wajumbe wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji ni 161. Kwa upande wa
Kinondoni kuna wajumbe 58 ambapo CCM wapo 20 na ukawa 38.
Temeke jumla ya wajumbe 49, CCM wapo 31 na ukawa 18 na Ilala jumla ya wajumbe 54 huku CCM wakiwa 23 ukawa 31.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment