SERIKALI imeagiza ulipaji wa ushuru wa
huduma unayofanywa na migodi mbalimbali nchini ufanyike hadharani ili
kila mwananchi aelewe kiasi kilicholipwa.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa
Sospeter Muhongo alitoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara kwenye
mgodi wa dhahabu wa Cata Mining uliopo katika kijiji cha Kataryo,
mkoani Mara ambako alikagua shughuli za mgodi huo na kuweka jiwe la
msingi.
Profesa Muhongo alisema ili kuondoa
hali ya sintofahamu pamoja na kuongeza uwazi na utekelezaji sahihi wa
miradi kutokana na fedha zitokanazo na malipo ya ushuru wa huduma, ni
lazima ulipaji huo wa ushuru husika ukashuhudiwa na kila mwananchi.
Waziri Muhongo alimuagiza Kamishna wa
Madini kuandika barua kuikumbusha migodi yote nchini pamoja na
halmashauri ambazo kuna migodi kufuata utaratibu uliowekwa. “Migodi
itaandaa mfano wa hundi ya malipo husika na italipa hadharani kwenye
mikutano ya hadhara ili kila mwananchi wa eneo husika ashuhudie, na
aelewe kiasi halisi kilicholipwa,” alisema.
Aidha aliongeza:“Asilimia 0.3
inayolipwa kama ushuru wa huduma ni lazima iende kwenye miradi ya
maendeleo ya maeneo husika na sio vinginevyo, ” alisisitiza.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MUHONGO: MIGODI ILIPE USHURU HADHARANI
Reviewed by Newspointtz
on
15:27:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment