Mpekuzi blog
Siku
chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kuwasimamisha
kazi wauguzi watano wa Hospitali ya Butimba wilayani Nyamagana Mkoani
Mwanza kufuatia uzembe uliopelekea vifo vya watoto mapacha, madaktari wa
hospitali hiyo jana waligoma kwa saa kadhaa.
Madaktari
hao waligoma kutoa huduma kwa zaidi ya saa sita na kusababisha usumbufu
mkubwa, wakidai kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na kutishwa na watu
wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.
Akieleza
sababu ya mgomo huo, Bi. Rechungula ambaye ni mmoja kati ya watoa
huduma ya afya katika hospitali hiyo alisema kuwa wagonjwa wamekuwa
wakikiuka taratibu za kupata huduma huku wakiwatishia na kuwasukuma
kufanya kazi zao.
“Wagonjwa
wanakuja hawataki kufuata utaratibu, wakifika mlangoni wanataka
kuandikiwa kadi mara moja bila kufuata utaratibu. Na wakifika kwa
daktari vivyo hivyo." Alisema Bi. Rechungula
Alisema kuwa wagonjwa wamekuwa wakiwatishia kuwapiga endapo hawatawahudumia kwa muda wanaoutaka.
Kufuatia
sakata hilo, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga alifika
hospitalini hapo na kuwahakikishia usalama wauguzi hao, huku
akitahadharisha watu wanaotaka kuhatarisha usalama.
Alisema
kuwa hakutakuwa na sababu ya kuweka ulinzi wa polisi kusimamia huduma
hospitalini hapo bali hali ya amani inapaswa kuzingatiwa.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment