Shule
ya msingi mhola iliyopo katika kitongoji cha v/60 B ,Tarafa ya Ifakara wilayani
kilombero inakumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa madawati na
matundu ya vyoo.
Akizungumza
na newspointtz.blogspot.com ofisini
kwake jana kwa niaba ya Mkuu wa shule mwalimu wa taaluma Mariam Magali alisema
kuwa wanakumbana na changamoto mbalimbali kama
upungufu wa madawati hali ambayo inapelekea baadhi ya wanafunzi wanakaa chini.
Aidha
Magali alisema sio madawati pekee bali na upungufu wa matundu ya vyoo hali
ambayo inapelekea walimu na wanafunzi kuchangia vyoo pamoja na upungufu wa
madarasa haliambayo inapelekea wanafunzi kufanya zamu katika ufundishwaji.
“Wanafunzi
ni wengi kiasi ambacho kinapelekea kufanya zamu ya kuwafundisha hali inayotupa
wakati mgumu kama walimu kutimiza majukumu ya
kikazi”alisema Magali
Sanjari
na hayo mmoja kati ya wazazi aliyejulika kwajina la saddam kallesi ambae mtoto
wake anasoma katika shule hiyo alisema kuwa wazazi ambao bado hawaja
waandikisha watoto wao wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Hata
hivyo magali ametoa wito kwawadau mbalimbali waelimu wakishilikiana na kamati
ya shule kufanya kila njia zabkutatua changamoto hizo shuleni hapo, pia
amewaasa wazazi wapewe elimu kuhusu suala la elimu bure
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
MAGALI:Madawati,matundu ya vyoo ni changamoto Mhola
Reviewed by Newspointtz
on
07:27:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment