Mbunge wa jimbo la Kilombero Mh.Peter Lijualikali (aliyevaa suti)katika moja ya matukio aliyowahi kukamatwa.picha na maktaba |
Jeshi la Polisi Mkoani
Morogoro, wilayani Kilombero jana lilimkamata mbunge wa jimbo la
Kilombero (Chadema), Peter Lijualikali kwa madai ya kutaka kuingia katika kikao
cha Baraza la Madiwani cha kuapisha na kuchagua mwenyekiti na makamu wake
wakati si mpigakura.
Lijualikali alikamatwa nje ya
ukumbi wa halmashauri na polisi na kuswekwa rumande katika Kituo Kikuu cha
Polisi Wilaya ya Kilombero saa 3.48 asubuhi wakati akiingia kwenye ukumbi huo kama mmoja wa mashuhuda.
Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya
Kilombero, Shabaan Mikongolo alisema mbunge huyo hakutendewa haki na polisi kwa
kuwa alifika eneo hilo
kushuhudia matukio ya kuapishwa kwa madiwani.
“Ni kama kuna maelekezo
yalitolewa kwa polisi kuwazuia wabunge, Lijualikali na Devotha Minja (Viti
Maalumu – Chadema) na mwakilishi wa Katibu Mkuu Chadema kutoingia ukumbini
lakini viongozi wengine wa Serikali ngazi ya mkoa na wilaya waliruhusiwa."
Alisema Mikongolo
Pia, polisi walizuia waandishi wa
habari na kutaka kuwanyang’anya kamera zao kwa sababu ambazo hazikuwekwa
bayana.
Katika uchaguzi huo, Diwani wa
Sanje (CCM), David Ligazo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Kilombero kwa kura 19 dhidi ya Godfrey Lwena ( CHADEMA) aliyepata kura 18
Chanzo.Mpekuzi
0 comments:
Post a Comment