Ligi
ya Mabingwa barani Ulaya, iliyochezwa usiku wa jana Jumatano kwenye
viwanja viwili tofauti, ikiwemo uwanja wa Stamford Bridge uliyopo
jijini London na Petrovsky uliopo nchini Urusi .
Jiji
la London, dakika chache zilizopita wenyeji Chelsea wamelazimika
kuchezea kichapo cha pili mfululizo toka kwa PSG kutoka jijini Paris
nchini Ufaransa kwa kufungwa bao 2-1, ambapo ushindi huo ni kama ule
walioupata timu hiyo ya PSG katika mchezo wao wa awali na kwa maana
hiyo, PSG wameweza kujipatia pointi 6 muhimu na magoli 4, huku Chelsea
wao wakiambulia mabao yao 2.
Kwa
hatua hiyo, PSG anaingia hatua ya robo fainali katika michuano hiyo
mikubwa kabisa barani Ulaya..PSG ilikuwa inahitaji ushindi wa aina
yoyote ili kuweza kusonga mbele au sare, hivyo kwa ushindi huo imefuzu
hatua ya robo fainali.
Mchezo mwingine umechezwa nchini Urusi , wenyeji Zenit wameweza kulala kwa bao 2-1 dhidi ya Benfica ya nchini Ureno.
Katika
mchezo wa awali Benfica walikuwa nyumbani na walifanikiwa kushinda bao
1-0, kwa hatua hiyo Benfica wamefanikiwa kuingia hatua ya robo ya
michuano hiyo kwa jumla ya poiti 6 huku ikijipatia mabao 3, dhidi ya
moja la wapinzani wao hao.
Taarifa hizi ni kwa msaada wa Mashirika ya Habari na kuandaliwa na Andrew Chale
Mchezaji wa PSG, Ibrahimovic akipachika bao wavuni..dhidi ya Chelsea usiku huu na kufanya matokeo 2-1.
Mchezaji wa PSG, Ibrahimovic akishangilia bao lake aliloifungia PSG dhidi ya Chelsea usiku huu na kufanya matokeo 2-1.
0 comments:
Post a Comment