NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

MENEJA WA DIAMOND AWEKA WAZI SABABU ZA KUFANYA KAZI NA AY

 

Baada ya msoto na hatimaye kufanikiwa kimuziki Ambwene Yesaya AY ametangaza rasmi kumpata mtu atakayesimamia kazi zake (Meneja) ambaye ni Sallam SK meneja mahiri kabisa wa masuala ya nje wa msanii nyota Diamond Plutnumz.
 

Meneja huyo wa Diamond Salaam SK katika mahojiano yake na kituo cha East Africa Radio amesema  licha ya Ay kuwa na Connections za kutosha pamoja kujisimamia mwenyewe mda mrefu,ameamua kufanya naye kazi kwasababu ya uwezo mkubwa alionao wa kushawishi kufanya kazi na watu mbalimbali.

Salaam amesema kuwa na connection ni jambo moja na kuweza kuzishawishi connections hizo ni jambo la pili, ingawa haimaanishi AY hawezi lakini amemuamini yeye kwajinsi alivyoona ushawishi wake.

Pia Salaam ameongeza kuwa katika menejiment yake hafanyi kazi na mtu ambaye hajitumii katika kazi zake na kuongeza kuwa msanii lazima awe na ushawishi kwa meneja wake na kumlazimisha kufanya vitu ambavyo meneja akiona hawezi kuamini kama vingefanikiwa, akiwa na maana ya wivu wa maendeleo.

chanzo>mtembezi

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

2 comments: