MKUU
wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Davis Mwamunyange, amemtumia
salamu za pongezi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa tena na wananchi wa Zanzibar
kushika wadhifa huo kwa muhula wa pili cha madaraka.
Salamu
hizo zilizotumwa na Jenerali Mwamunyange kwa niaba ya Maofisa, Askari
na Watumishi wa Umma wanaofanya kazi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ), zilieleza kuwa ushindi wa kishindo wa Dk Shein
alioupata unadhihirisha kuwa wananchi wa Zanzibar wameridhishwa na
uongozi wake makini na mahiri aliouonesha katika muhula wake wa kwanza
wa uongozi wake.
Salamu
hizo ziliendelea kueleza kuwa historia ya Dk Shein ya uaminifu, maadili
mema na uzalendo aliouonesha katika utumishi wake wa muda mrefu katika
nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika kabla hajawa Rais wa Zanzibar
imewapa wananchi imani kubwa kuhusu uongozi wake.
“Mheshimiwa
Rais, hapana shaka kuwa katika muhula huu wa pili wa uongozi wako,
Zanzibar itashuhudia mafanikio makubwa zaidi ya maendeleo ya kiuchumi na
kijamii, sambamba na kuendelea kuwepo kwa hali ya amani na utulivu kwa
wananchi wote,” ilieleza sehemu ya salamu hizo.
Aidha,
salamu hizo za pongezi zilieleza kuwa JWTZ inamhakikishia Dk Shein kuwa
itaendelea na utiifu, uadilifu na uaminifu mkubwa kwake kama ilivyo
desturi ya majeshi nchini. W
akati
huo huo, Rais mstaafu wa Awamu ya Pili Zanzibar, Abood Jumbe Mwinyi,
naye amemtumia salamu za pongezi Dk Shein kwa ushindi wa kishindo
alioupata katika marudio ya uchaguzi wa Zanzibar.
Kwa
niaba yake na familia ya Mzee Jumbe, salamu hizo zilitoa pongezi kwa Dk
Shein pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ushindi huo na kueleza
furaha yake ya moyoni mwake kwa kuona jinsi alivyokiwakilisha chama cha
CCM na kukipatia ushindi ambao ulitegemewa.
Nao
uongozi na wanachama wa ‘Veteran Young Pioneer Association Zanzibar’
umetoa salamu za pongezi kwa Dk Shein kutokana na ushindi wa kishindo
alioupata wa kura 299,982 sawa na asilimia 91.4 katika Uchaguzi Mkuu wa
Marudio uliofanyika hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment