NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

NAPE AFANYA YAKE UZINDUZI WA VIDEO YA SIZONJE YA MRISHO MPOTO



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye Jumamosi hii katika ukumbi wa Golden Jubilee Tower (PSPF Tower) jijini Dar es salaam amepamba uzinduzi wa video mpya ya wimbo ‘Sizonje’ wa Mrisho Mpoto.

 Uzinduzi huo uliambatana na mdahalo wa kuwatia moyo wanafunzi waliofeli kidato cha nne ambapo wazungumzaji mbalimbali kama Waziri Nape Nnauye, Mtangazaji maarufu wa radio ya Clouds FM Millard Ayo, Mkurugenzi wa vipindi na Uzalishaji wa Clouds FM Ruge Mutahaba, Mrisho Mpoto pamoja na wanafunzi waliofeli na waliofaulu, waliweza kuzungumzia dhana ya kufeli shule sio mwisho wa maisha

Akizungumza na wadau waliyojitokeza katika uzinduzi huo, Mh Nape alisema anafurahishwa na jinsi Mrisho Mpoto anavyoweza kuitumia sanaa yake kwa ajili ya kuijenga jamii.

“Hii kazi anayofanya Mpoto ndio kazi yangu, kwa hiyo lazima aungwe mkono,” alisema Nape huku akimwagia sifa msanii huo ambaye kwa sasa yupo kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za KORA kama wasanii bora wa muziki wa asili Afrika

Pia Nape aliendesha harambee ndogo ya kuuza DVD mpya za video ya wimbo Sizonje na kufanikiwa kuuza zaidi ya DVD 7 kwa milioni nane na nusu huku mwenyewe akinunua moja kwa milioni 2. Angalia picha.

 chnzo>mtembezi

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment