MBUNGE wa Sengerema, William Ngeleja,
amempongeza Rais John Magufuli kwa kuanza kutekeleza ahadi yake ya
ujenzi wa daraja la kisasa kwenye kivuko cha Kigongo –Busisi lenye urefu
wa mita 3,200 wilayani Sengerema.
Alitoa pongezi hizo jana wilayani humo,
alipozungumza na wanahabari kuhusu utekelezaji wa ahadi za Rais
alizozitoa wakati wa kampeni ya Uchaguzi Mkuu. Alisema,
Rais ametoa Sh milioni 700 zitakazotumiwa na Mkandarasi Mshauri kufanya
upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo, ambalo kwa mujibu
wake litakuwa ni la kwanza na la aina yake kuwahi kujengwa kwa nchi za
Kusini mwa Jangwa la Sahara.
“ Kwa niaba ya wananchi wa Sengerema
nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Rais wetu kwa kuanza kutekeleza
moja ya ahadi muhimu aliyowaahidi wananchi wa Sengerema ya ujenzi wa
daraja la kisasa kwenye kivuko cha Kigongo- Busisi,” Ngeleja alisema.
Alisema, Serikali imekwishatangaza
zabuni ya kuanza kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa daraja
hilo, jambo lililowapa faraja wakazi wa Sengerema na mikoa ya jirani.
Alisema, daraja hilo litakapokamilika litaharakisha shughuli za
maendeleo ikiwa ni pamoja na kusaidia kukuza uchumi wa wananchi na
kuondokana na umasikini wa kipato.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
NGELEJA AMPA ‘BIG UP’ RAIS MAGUFULI
Reviewed by Newspointtz
on
07:14:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment