Mahakama ya Haki za Binadamu ya Afrika
(AfCHPR) katika kikao chake kilichofanyika majuma kadhaa yaliyopita
jijini Arusha, ilipitia maombi ya rufani ya mwanamuziki maarufu nchini,
Nguza Viking na John Viking dhidi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hata hivyo, taarifa iliyotolewa na
mahakama hiyo, ilieleza kuwa kesi hiyo namba 006/2015 iliyopangwa
kusikilizwa Machi 11 haitasikilizwa katika mahakama ya wazi.
Ni kesi mbili pekee kati ya 50
zitakazosikilizwa kwenye mahakama ya wazi, ikiwamo inayomhusu mwanasiasa
maarufu wa Rwanda, Victoire Ingabire aliyoifungua kupinga ukiukwaji wa
haki anaofanyiwa na Serikali yake.
Mahakama hiyo inaundwa na majaji 11
kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) na inakuwa na vikao vinne
kwa mwaka, kufikia Januari 31 tayari ilikuwa imepokea kesi 74 kati ya
hizo 25 imetolewa uamuzi.
Maombi manne yamepelekwa kwa uamuzi zaidi kwenye Kamisheni ya Afrika ya Haki za Binadamu.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
RUFAA KESI YA BABU SEYA KUSIKILIZWA LEO MACHI 11, 2016
Reviewed by Newspointtz
on
07:07:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment