NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

PSG yamvizia Sturridge

 
MATAJIRI wa Ufaransa, Paris Saint-Germain wanaitaka huduma ya mchezaji mwenye thamani ya Pauni Milioni 45, mshambuliaji wa Liverpool, Daniel Sturridge.
 
Msafara kutoka klabu hiyo ya Paris unatarajiwa kuwasili London kuhudhuria mechi kati ya England na Uholanzi Uwanja wa Wembley leo.
 
Sturridge anatarajiwa kucheza sehemu ya mchezo huo baada ya kurejeshwa kikosini. Kocha wa PSG, Laurent Blanc atakuwa sokoni kusaka mshambuliaji mpya kutokana na Zlatan Ibrahimovic na Edinson Cavani kuhofiwa kuwa mbioni kuondoka.

Na Sturridge jina lake limo katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa PSG, ingawa amebakiza miaka mitatu katika Mkataba wake Merseyside.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment