Nhodha
wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, John Bocco
‘Adebayor’, amesema kuwa bado wataendelea kupambana katika Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara (VPL) na Kombe la Shirikisho Afrika ili kutimiza
malengo waliyojiwekea.
Azam
FC inayodhaminiwa na Benki bora kabisa nchini ya NMB, imejiwekea
malengo ya kutwaa ubingwa wa VPL msimu huu pamoja na kufika hatua ya
makundi (robo fainali) ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka
huu.
Mabingwa
hao wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati (Kombe la CECAFA
Kagame), mwishoni mwa wiki iliyopita waliitoa Bidvest Wits ya Afrika
Kusini kwa jumla ya mabao 7-3 kwenye raundi ya kwanza ya Kombe la
Shirikisho Afrika na sasa itakutana na Esperance katika raundi pili ya
michuano hiyo.
Mchezo wa kwanza dhidi ya Esperance utafanyika Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kabla ya ule wa marudiano kupigwa wiki moja baadaye jijini Tunis.
Mchezo wa kwanza dhidi ya Esperance utafanyika Aprili 10 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam kabla ya ule wa marudiano kupigwa wiki moja baadaye jijini Tunis.
Katika
VPL Azam FC inashika nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi
50 sawa na Yanga iliyo nafasi ya pili kwa tofauti nzuri ya mabao ya
kufunga na kufungwa (GD), lakini inazidiwa mechi tatu za kucheza kama
Yanga dhidi ya Simba iliyokileleni kwa pointi
Bocco
aliwahakikishia mashabiki wa Azam FC kuwa watazidi kupambana hadi
dakika ya mwisho na kuhakikisha timu hiyo inafika mbali zaidi kwenye
michuano hiyo.
“Tunamshukuru
Mungu tumeweza kuvuka na kwenda kwenye hatua nyingine, tunachowaahidi
mashabiki wetu tutaendelea kupambana katika ligi pia michuano ya
kimataifa na kufika mbele zaidi,” alisema.
Bocco
amefunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi zote dhidi ya Bidvest,
akifunga moja jijini Johannesburg waliposhinda mabao 3-0 mengine
yakitupiwa na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Shomari Kapombe, kabla ya
nahodha huyo kupiga jingine walipowararua Wasauzi hao 4-3 ndani ya
Uwanja wa Azam Complex, mchezo ulioshuhudiwa Kipre Tchetche akifunga
hat-trick (mabao matatu).
0 comments:
Post a Comment