Newspointtz blog
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Balozi Eng. John William Herbert Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu
jijini Dar es Salaam. Balozi Kijazi anachukua nafasi ya Balozi Ombeni
Sefue ambaye atapangiwa kazi nyingine.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha
Balozi Mhandisi John William Kijazi kuwa Katibu Mkuu Kiongozi.
Hafla
ya kuapishwa Balozi Kijazi imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mheshimiwa
Kassim Majaliwa, Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, Makatibu wakuu
na Naibu Katibu Wakuu.
Balozi
Kijazi ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa
Balozi wa Tanzania nchini India, anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue
ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wakati
huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ameagana na Mwakilishi wa Shirika Ia Umoja wa Mataifa Ia
kuhudumia wakimbizi hapa nchini (UNHCR) anayemaliza muda wake Bi. Joyce
Mends-Cole Ikulu Jijini Dar es salaam, ambapo pamoja na mambo mengine
amemshukuru kwa kazi kubwa ya kuhudumia wakimbizi kwa kipindi chote
alichokuwepo hapa nchini.
Kwa
upande wake Bi. Joyce Mends-Cole amempongeza Rais Magufuli kwa kazi
nzuri inayofanywa na Tanzania kuzisaidia nchi zenye matatizo, hususani
migogoro ya kisiasa ambayo husababisha watu wake kuwa wakimbizi.
Pia
amepongeza kuteuliwa kwa Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mheshimiwa
Benjamin William Mkapa, kusaidia usuluhishi wa mgogoro wa Burundi ambao
umesababisha idadi kubwa ya wakimbizi kukimbilia Tanzania.
Hata
hivyo amesema idadi ya wa kimbizi wanao kimbilia Tanzania imepungua
kutoka wakimbizi 3,000 waliokuwa wakiingia hapa nchini kwa wiki, wakati
Mgogoro wa Burundi ulipoanza hadi kufikia wakimbizi takribani 1,000
wanaingia hapa nchini kwa wiki hivi sasa.
Aidha,
Bi. Joyce Mends-Cole amewashukuru watanzania kwa ushirikiano alioupata
kwa kipindi cha miaka mitatu aliyofanya kazi hapa nchini, na ameahidi
kuwa Balozi wa kuitangaza vyema Tanzania.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
07 Machi, 2016
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri
Mkuu Kassimu Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William
Herbert Kijazi wa kwanza kushoto na Wa mwisho kulia ni aliyekuwa Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William
Herbert Kijazi aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue pamoja
na viongozi Wakuu wa Ulinzi na Usalama nchini.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi
pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha tukio
la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John William Herbert Kijazi
pamoja na Manaibu Katibu Wakuu wa Wizara mbalimbali mara baada ya kuisha
tukio la Uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam.PICHA NA IKULU
0 comments:
Post a Comment