NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

RC Makonda Amtembelea Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo,kupiga goti


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameanza ziara ya kuwatembelea wazee na viongozi wa dini ili kupata busara zao  ambapo jana alimtembelea  Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo  kwa  ajili  ya  kupata  baraka  na  busara  zake

Siku chache baada ya kuapishwa, Machi 19, mwaka huu alikutana na wenyeviti na watendaji wa mitaa 559 wa Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu huyo wa mkoa alitumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa viongozi hao ili afanye nao kazi kwa ushirikiano na kuja na mikakati tisa, ikiwamo kutenga maeneo ya biashara kwa lengo la kuifanya Dar es Salaam kuwa ya kisasa.

Akizungumza jana, alisema lengo la ziara hiyo ni kujifunza na kuchukua busara kutoka kwa wazee ili zimsaidie katika utendaji wake.
“Mkoa huu una wazee. Ili uweze kuongoza vyema ni lazima upate busara zao zikusaidie katika majukumu yako,” alisema Makonda ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa mkoa, leo anatarajia kukutana na Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry na Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
Kadinali Pengo akiwa kwenye mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ofisini kwake makao makuu ya Kanisa Katoliki, Forodhani jijini  jana     
 chanzo>mpekuzi

 
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment