WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto imetangaza kuiunga mkono Polisi nchini katika
operesheni ya kukamata wateja wa makahaba kuhakikisha biashara hiyo
inakoma nchini.
Waziri wa wizara hiyo, Ummy Mwalimu
alisema takwimu zinaonesha wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa
wa Ukimwi, ambapo kati ya Watanzania 100 wanaopimwa, sita ni wanawake na
wanaume ni wanne pekee.
Akizungumza
katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Dar es Salaam jana, Ummy
alisema si haki kuwakamata wanawake wanaojiuza na kuwaacha wateja wao
ambao ni wanaume.
“Ninalipongeza Jeshi la Polisi kwa
hatua hiyo kwa sababu imeonesha kutoegemea upande mmoja kwa kuwakamata
wanawake makahaba. Wote wanaojiuza na wanaonunua huduma hiyo ni wakosaji
wanaostahili kuchukuliwa hatua za kisheria.
Tunaungana na Polisi kushiriki
operesheni hiyo,” alisema. Alieleza kuwa, biashara ya ukahaba
inayofanywa na wanawake isingekuwepo endapo wateja wasingekuwepo, hivyo,
wateja wanastahili kukamatwa pia kwa sababu ndio wanaoichochea.
Ummy alisema familia nyingi zina
misukosuko na wanawake wengi wamekuwa wakiteseka na wengine kuambukizwa
magonjwa na waume zao wanaoshiriki biashara hiyo. Katika hatua nyingine,
alisema sasa wanataka kuona idadi ya wanaume wateja wa biashara hiyo
inatajwa sambamba na ya wanawake wanaokamatwa nao ili ndugu na wake zao
wafahamu kuhusu tabia yao hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said
Mecky Sadiki, alisema hatua ya kukamata wateja na wauza miili imetokana
na makubaliano yaliyofikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Dar es
Salaam.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
SASA UKAHABA NCHINI BASI
Reviewed by Newspointtz
on
11:35:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment