Serikali imeanza mazungumzo na Ubalozi wa Malawi nchini baada ya nchi hiyo kuteketeza tani 2.6 za meno ya tembo yaliyotoka Tanzania.
Serikali
inafanya mazungumzo hayo ili kuzuia kuchomwa kwa meno mengine yaliyopo
nchini humo kwa kuwa ni kielelezo kinachohitajika mahakamani.
Mkurugenzi
wa Wanyamapori wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Herman Keraryo alisema
mwanasheria wa wizara alifanya mawasiliano na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali na ubalozi huo ili kuwasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Malawi.
Idadi ya vipande vya meno ya tembo vilivyokamatwa nchini Malawi ni 781 na thamani yake inakisiwa kuwa bilioni 3.
Idadi ya vipande vya meno ya tembo vilivyokamatwa nchini Malawi ni 781 na thamani yake inakisiwa kuwa bilioni 3.
chanzo>mpekuzi
0 comments:
Post a Comment