NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

MAN CITY YATINGA ROBO FAINALI ULAYA


Man City-rekodi
Manchester City wamefanikiwa kufuzu kucheza robo fainali ya michuano ya Champions League  kwa mara ya kwanza licha ya kutoka sulusu kwenye mchezo wao wa marudiano dhidi ya Dynamo Kiev jana usiku.
City ilishinda kwa bao 3-1 kwenye mchezo wa awali, walianza vyema mchezo huo lakini wakajikuta wakiwakosa walinzi wao nguzo wa kati Vincent Kompany na Nicolas Otamendi dakika za mapema baada  ya kuanza kwa mchezo huo kutokana na kupata majeraha na kushindwa kuendelea na mchezo.
Hadi kipindi cha kwanza inamalizika hakuna timu ambayo ilikuwa imepiga hata shuti moja on target. Jesus Navas alipiga shuti ambalo liligonga mwamba wakati shuti la Yaya Toure likiokolewa na mlinda mlango wakati wa kipindi cha pili.
Rekodi zilizowekwa na Man City
  • Manchester City ni timu ya saba nyingine tofauti kuingia robo fainali ya Champions League kutoka England baada ya Arsenal, Tottenham, Leeds, Liverpool, Manchester United pamoja na Chelsea tangu mwaka 1992
  • Man City wameweka rekodi ya kucheza mechi 10 bila kuruhusu nyavu zao kutikiswa kwenye michuano hiyo ya Ulaya mara ya mwisho ilikuwa ni December 2014 dhidi ya Roma.
  • Mchezo wa jana usiku ulikuwa ni wa pili Manchesyer City inacheza dakika 90 bila kupata bao kwenye michuano ya Champiuons League ndani ya uwanja wa Etihad
  • City waliweza kupiga shuti moja tu on target wkati wa mchezo, shuti hilo lilipigwa dakika ya 73 kipindi cha pili.
Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment