MABAO ya dakika 75 na 90, yaliyofungwa
na Simba leo jioni yameisaidia timu hiyo kupanda kileleni mwa msimamo wa
Ligi Kuu Bara na kuzishusha timu za Yanga na Azam, zilizokuwa kileleni.
Simba iliyocheza mchezo huo kwenye
Uwanja Taifa jijini Dar es Salaam, ilishuhudia mabao yake yakifungwa na
Danny Lyanga na Ibrahim Ajib.
Mchezo huo ulioanza kwa kasi ulishuhudia
Mbeya City wakipoteza nafasi ya kufunga bao dakika ya tatu baada ya
kupokea pasi kutoka kwa Haruna Moshi ‘Boban’.
Simba ilijibu shambulio hilo dakika ya
tano baada ya mshambuliaji wake Ibrahim Ajib, kukosa bao la wazi
akishindwa kuunganisha mpira wa Hamis Kiiza ‘Diego’.
Mchezo huo ambao Mbeya City walicheza
offside trick, kipindi cha kwanza ulishuhudia Kiiza, akikosa bao la wazi
baada ya kupiga mkwaju nje ya 18 na mlinda mlango wa Mbeya City,
Hannington Kalysebula kuudaka.
Dakik ya 28 Mbeya City, walipata mkwaju
wa adhabu ndogo ambao ulienda kupigwa na Haruna Shamte na mpira huo
kugonga mwamba wa juu.
Mchezo uliokuwa na mashambulizi ya kushitukiza kwa pande zote, ulishuhudia ukienda mapumziko bila timu kupata bao.
Mchezo huo ukikaribia kwenda mapumziko
uliwashuhudia mabeki wa Simba Emiry Nimubona na Juuko Mursheed,
wakijichanganya katika kuokoa mpira na Geofrey Mlawa, kushindwa
kuifungia bao Mbeya City.
Simba walirudi kipindi cha pili na
kufanya mabadiriko ya wachezaji kadhaa ili kuhakikisha wanapata bao,
huku mashabiki wa timu hiyo wakilizomea benchi la ufundi kutaka
mabadiriko ya wachezaji.
Dakika ya 71, kulitokea mashambulizi ya
timu zote kwa Mbeya City nahodha wao Kenny Ally, kupiga mkwaju mkali
ambao ulidakwa na Vincent Agban, huku dakika ya 72, Hassan Kessy wa
Simba akipanda na mpira na kuchonga krosi iliyoshindwa kutumiwa vyema na
Danny Lyanga.
Simba, ilijipatia bao hilo pekee baada
ya kaazi nzuri iliyofanywa na kiungo mshambuliaji Awadh Juma, aliyeingia
uwanjani kipindi cha pili akichukua nafasi ya Kiiza.
Mabadiriko ya kipindi cha pili
yaliyofanywa na kocha wa Simba, Jackson Mayanja, ndio yaliyoongeza
presha katika lango la Mbeya City na Simba kupata ushindi huo.
Simba: Vincent Angban, Nimubona / Hassan
Kessy, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, Mursheed, Novatus Lufunga, Justice
Majabvi, Jonas Mkude, Brian Majwega / Danny Lyanga, Mwinyi Kazimoto na
Kiiza / Awadh Juma.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
SIMBA YAITUNGUA MBEYA CITY AREJEA KILELENI VPL
Reviewed by Newspointtz
on
19:38:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment