Rapa mahiri nchini Chidbenz ameweka wazi
kuwa Rapa kutoka mkoani Morogoro Stamina alikuwa anamfuatilia na
kumkubali sana kiasi cha kujiita Chidbenz enzi hizo kule kwao nakuongeza
kuwa watu wengi wanalitambua suala hilo lakini alikuja kubadili
mwelekeo baada ya kuona Chidbenz kapotea kwenye ramani ya muziki.
Akizungumza
na Planet Bongo ya East Afrika Radio Chid amesema siku hizi watu
wanamuona Stamina akisema kuwa rapa FID Q ndiye rapa anaye mkubali zaidi
lakini haikuwa hivyo toka zamani.
Chidbenz
amefafanua zaidi na kueleza kuwa Skendo zake za kutumia dawa za
kulevya,kufunggwa jela na kupotea kwenye ramani ya muziki ndiko
kulimfanya Stamina kutoona sababu ya kujivunia kwake kwahiyo akahamia
kwa rapa Fid Q.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
SKENDO ZA CHIDBENZ ZABADILI MSIMAMO WA STAMINA
Reviewed by Newspointtz
on
15:33:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment