Usiku wa Ulaya umerejea baada ya wiki mbili kupita ikiwa ni michezo ya pili hatua ya 16 bora kuelekea robo fainali baada michezo ya kwanza kupigwa, hizi ni takwimu kadhaa za mchezo wa leo kati ya Real Madrid Vs AS Roma.Kabla ya msimu huu klabu hizi zilishakutana mara nane katika mashindano ya UEFA, Madrid ikishinda mara 4 dhidi ya mara 3 kwa Roma na kutoka sare mara moja.
Timu hizi zilikutana katika maandalizi ya msimu mpya kwenye mchezo wa kirafiki mjini Melbourne tarehe 18 Julai mwaka jana. Roma walishinda 7-6 kwa penalti baada ya sare ya 0-0, Seydou Keita akipiga penati ya ushindi baada ya Morgan De Sanctis kupiga mkwaju uliookolewa na mlinda mlango Lucas Vázquez.Mara ya mwisho kukutana kwenye Uefa Champions League kabla ya mwaka huu ilikua ni hatua 16 mwaka 2007/08 wakati Roma ikiweka kumbukumbu ya ushindi wa 2-1 nyumbani na ugenini.
Mechi ya kwanza ilipigwa Stadio Olimpico na Raúl González alifunga bao la kuongoza kabla ya David Pizarro na Mancini kusawazisha na kuongeza bao la pili hivyo kufanya mchezo wa kwanza kuisha kwa ushindi huo wa Roma wa 2-1.Raúl alifunga tena katika mechi ya pili bao la kwanza lakini alikuwa ni Rodrigo Taddei aliyesawazisha bao hilo kabla ya Ppe wa Madrid kutolewa kwa kadi nyekundu ndipo Mirko Vucinic alipopiga bao la pili na kufanya jumla ya matokeo kuwa 4-2 na rom wakasonga mbele.
Wakati huo vikosi vilikuwa hivi,
Real Madrid: Casillas, Salgado (Torres 64), Pepe, Cannavaro, Heinze, Diarra (Drenthe 61), Gago, Guti, Julio Baptista (Soldado 85), Robinho, Raúl.
Roma: Doni, Cicinho (Panucci 87), Mexès, Juan, Tonetto, Aquilani, De Rossi, Perrotta (Pizarro 76), Taddei, Mancini (Vucinic 65), Totti.
Wiki mbili zilizopita timu hizi ilikutana kwenye hatua hii ya 16 Msimu wa 2015/2016, Madrid wakianzia ugenini na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, Swali je Roma ataweza kupindua matokeo na kusonga mbele? Majibu utayapata hapa hapa baada ya mchezo utakaopigwa majira ya 22:45 Usiku.
MICHEZO YA LEO
Real Madrid |
v |
Roma |
Santiago Bernabeu |
22:45 |
|
VfL Wolfsburg |
v |
KAA Gent |
Volkswagen Arena |
22:45 |
0 comments:
Post a Comment