Spika
wa Bunge la Tanzania, Mhe. Job Ndugai leo amekuwa mgeni rasmi katika
ufunguzi wa mkutano unaohusisha baadhi ya wabunge wa bunge la Tanzania
na wadau wa afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akizungumza na Mtaalamu Mwandamizi wa
Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya. Bw.Svend Robinson.
Walikuwa wakizungumza kabla ya kuanza kwa mkutano uliowahusisha baadhi
ya Wabunge na wadau wa Afya. Mkutano huo ulilenga kujadili kuhusu
uwekezaji katika Sekta ya Afya na ulifayika leo tarehe 3 Machi, 2016
Jijini Dar es Salaam.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akisalimiana na baadhi ya wabunge
waliohudhuria mkutano wa pamoja na wadau wa Afya kujadaili kuhusu
uwekezaji katika sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai (wa pili kushoto), Naibu Waziri Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Hamis Kigwangala pamoja na
Mtaalamu Mwandamizi wa Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya
Bw.Svend Robinson wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta
ya Afya. Anayezungumza ni Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa nchi Dkt
Rufaro Chatora.
Baadhi ya Wabunge na Wadau wa Afya wakifuatilia mazungumzo juu ya uwekezaji katika sekta ya Afya hapa nchini.
Spika
wa Bunge Mhe. Job Ndugai akihutubia wadau mbalimbali wa Afya
waliokutana kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hapa nchini.
Spika
wa Bunge Mhe Job Ndugai (kushoto) Mwakilishi wa Shirika la Afya hapa
nchi Dkt Rufaro Chatora (katikakati) na na Mtaalamu Mwandamizi wa
Masuala ya Afya kutoka Mfuko wa Dunia wa Afya Bw.Svend Robinson
wakijadili jambo mara baada ya ufunguzi wa Mkutano uliowakutanisha wadau
mbalimbali wa Afya kujadili juu ya uwekezaji katika Sekta ya Afya hapa
nchini. (Picha na Ofisi ya Bunge)
0 comments:
Post a Comment