MAMLAKA
ya Mawasiliano nchini (TCRA) imeipiga faini ya milioni 10 kampuni ya
biashara ya mtandao – RIFARO AFRICA na pia imeizuia kuendelea na huduma
kwa madai ya kutokuwa na leseni.
Aidha
TCRA imeeleza kushangazwa na taarifa zinazotangazwa katika vyombo vya
habari na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa, kampuni hiyo
inafanya shughuli zake kutokana na leseni namba 178933 pamoja na cheti
cha TCRA namba 15420.
Akizungumza
hii leo Makao Makuu ya TCRA Dk. Ally Yahaya Simba Mkurugenzi, Mkuu wa
TCRA amesema, baada ya TCRA kuona taarifa hizo za upotoshaji, iliamua
kuihoji kampuni ya RIFARO na kuifanyia uchunguzi ambapo walibaini kwamba
haina uhalali.
“28
Julai 2014 TCRA ilitoa cheti cha matumizi ya rasilimali masafa kwa
ajili ya huduma ya ziada za mawasiliano kupitia SMS namba 15420 ili
kutengeneza mfumo wa kuunganisha taarifa za mawakala wao kuuza na
kusambaza muda wa maongezi kupitia wavuti.
“Cheti
hicho kilimalizika 27 Julai 2015 na kampuni hiyo haikuomba kibali tena
cha kuendesha biashara yoyote na hivyo inachokifanya sasa hivi ni
kinyume na kanuni ya 17(1) ya Mamlaka ya Mawasiliano ya Kielektroniki na
Posta ya mwaka 2011,” ameeleza Dk. Simba.
Ameongeza
kuwa, TCRA ilitumia sheria yake sura ya 172 kama ilivyorekebishwa na
kifungu cha 179 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta na
kuitaka kampuni hiyo ijitetee kwanini ischukuliwe hatua, ambapo ilikiri
makosa yake yote.
Makosa
ambayo RIFARO AFRICA imekiri katika shauri baina yake na TCRA mnamo 24
Februari 2016 ilipohojiwa ni pamoja na kufanya biashara bila kuwa na
kibali, kwani cheti namba 15420 kilikuwa kimeisha muda wake tangu Julai
2015.
Lakini
pia RIFARO imekiri kuingia mkataba wa kibiashara na kampuni ya Zanzibar
Telecom Limited (ZANTEL) kwaajili ya huduma ya Ezzy Pesa kama mtoa
huduma mkubwa “mobile money super dealer” kinyume na sheria.
“Kutokana
na makosa hayo tunaitaka RIFARO isitishe mara moja biashara
inayoiendesha kwa kutumia rasilimali namba 15420 kwani haina kibali
lakini pia tunaipiga faini ya shilingi milioni 10 za kitanzania kwa
kuendesha shughuli zake bila kibali”. Amesema Dk. Simba.
Mbali
na kampuni hiyo, TCRA pia imeshusha rungu kwa Kampuni ya Azam Marine
Company Limited ambayo inamilikiwa na mfanyabiashara Saed Salim
Bakhresa kwa kuitaka kuacha mara moja kuendesha shughuli za kiposta za
kusafirisha vifurushi na vipeto baada ya kubainika wanafanya hivyo bila
kuwa na leseni na kibali cha TCRA, hivyo kuikoseha serikali mapato
Vilevile TCRA imeipiga faini ya shilingi milioni 5 kampuni hiyo kutokana na kufanya shughuli hizo kinyume cha sheria
Vilevile TCRA imeipiga faini ya shilingi milioni 5 kampuni hiyo kutokana na kufanya shughuli hizo kinyume cha sheria
CHANZO:MPEKUZI
0 comments:
Post a Comment