Kufuatia
malalamiko kuhusu huduma duni za mitandao ya simu nchini, Mamlaka ya
Mawasiliano (TCRA) imezitoza faini kampuni kwa kushindwa kuwajibika
katika huduma zao.
Kampuni
za simu zilizopigwa faini kutokana na kutoa huduma mbovu ni pamoja na
Airtel, Smart, Tigo, Vodacom na Zantel. Pamoja na hivyo, zimetakiwa
kuboresha huduma zake ndani ya miezi sita.
TCRA
imefanya tathimini juu ya ubora wa huduma za mawasiliano ikiwemo sauti
na data zinazotolewa na kampuni hizo ambapo imebainika kutowatendea haki
watumiaji wake.
“TCRA
inazipiga faini kampuni hizi zinazoanzia milioni 12.5 mpaka milioni
27.5 na inazitaka kuboresha huduma zao, miezi sita tangu siku ya
kutolewa kwa tangazo hili,” imeeleza sehemu ya taarifa ya TCRA kwa vyombo vya habari.
Usumbufu
unaotajwa na TCRA ambao unafanywa na mitandao hiyo ni pamoja na kudai
namba haipatikani ilihali ipo hewani, kudai namba inatumika ilihali
sivyo, kukata salio la mteja pasipo ridhaa yake na kukatika kwa
mawasiliano mara kwa mara.
Kampuni
ya Vodacom ndiyo iliyopigwa faini kubwa zaidi (milioni 27.5) huku
Kampuni ya Smart ikipigwa faini ndogo zaidi (milioni 12.5), faini hizo
zimetozwa kulingana na ukubwa wa makosa ambayo kampuni husika imekuwa
ikiyafanya katika utoaji wa huduma zake.
Kampuni
ya Airtel imepigwa faini ya Sh. 22.5 milioni, Zantel Sh. 25 milioni na
Tigo Sh. 25 milioni. TCRA imezitaka kampuni hizo kulipa faini hizo
haraka iwezekanavyo na kuboresha huduma zao kabla ya mamlaka hiyo
kuchukua hatua kali zaidi.
Kwa
mujibu wa kifungu cha 17 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na
Posta Sura ya 306 mamlaka hiyo hapa nchini inayo mamlaka ya kutoa adhabu
kwa kampuni yoyote inayokiuka masharti ya leseni ya utoaji huduma.
CHANZO:MPEKUZI
0 comments:
Post a Comment