MAGARI 213 yanafuatiliwa na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) baada ya kubainika yameingizwa nchini bila
kulipiwa kodi na watu binafsi pamoja na taasisi mbalimbali zikiwemo za
dini. Miongoni mwa magari hayo, yamo yaliyoingizwa kwa misamaha ya Kituo
cha Uwekezaji (TIC) ambayo (misamaha) imetajwa kutumika isivyo.
Mamlaka imesema inafuatilia kuhakikisha
wahusika sanjari na waliosaidia ukwepaji huo wa kodi, wanachukuliwa
hatua. TRA imetaja majina na taasisi zinazohusika na uingizaji magari
hayo, kupitia matangazo kwa vyombo vya habari na imetoa siku nne
wajitokeze kulipia ushuru kabla ya hatua nyingine kuchukuliwa.
Ukaguzi
uliofanywa na mamlaka, ndiyo umebaini kuwepo kwa magari hayo
yaliyoingizwa nchini na kusajiliwa bila kufuata taratibu za forodha
hivyo kuyafanya yamilikiwe bila kulipiwa kodi stahili. Orodha ya magari
213 na namba za usajili, mmiliki na aina ya gari imetolewa katika vyombo
vya habari na mamlaka hiyo imewataka wahusika wajitokeze haraka kulipia
gharama hizo.
Baadhi ya kampuni, taasisi na watu
binafsi, wameingiza magari zaidi ya moja. Miongoni mwa taasisi
zilizotajwa kwenye orodha hiyo zenye magari zaidi ya moja ni JM Hauliers
Limited (26), Al-Jabri Co Ltd (16) na Kampuni ya Dhandho Road Hawlage
iliyoingiza 18.
Kampuni nyingine na idadi ya magari
yaliyoingizwa kwenye mabano ni Bamboo Rock Limited (7) na Dayosisi ya
Musoma, ambayo hata hivyo haikufafanuliwa ni ya madhehebu gani ya dini,
imeingiza magari manane. Wengine ni Fai Limited (3), Nam Transport
Company (6), Neni Enterprises (2) na Relief Partner International yenye
magari matatu.
Kwa upande wa watu binafsi wenye magari
zaidi ya moja yaliyoingizwa bila kulipia ushuru ni pamoja na Aloyce
Kajijira (6), Mohamed Masoud (5), Mwesige Rwiza (5), Nassor Zakaria (3),
Rumishaeli Shoo (3), Ruwaida Ally (4) Simon Mehi (2), Yahya Hilal (5)
na Zahor Issa mwenye magari matatu.
Wapewa siku nne Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi, Mkurugenzi wa Idara ya Huduma na Elimu kwa
Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo aliwataka wamiliki wa magari
yaliyoorodheshwa kufika katika ofisi zilizo karibu, wafanyiwe uhakiki
walipe ushuru stahiki kabla ya Machi 12 mwaka huu.
Alisema baada ya tarehe hiyo, TRA
itachukua hatua ya kufuatilia magari hayo na kuyakamata. Alisema
ufuatiliaji wa magari yaliyoingizwa nchini bila kulipiwa ushuru ni
endelevu. Waliouziwa matatani Akizungumzia watakaokuwa wameuziwa magari
hayo bila kufahamu kama yalitolewa bila kulipiwa kodi stahili, Kayombo
alisema pia wanatakiwa kujitokeza.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
TRA SASA KAZI NA MAGARI
Reviewed by Newspointtz
on
07:17:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment