WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ametoa siku tatu kwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB), awasilishe maelezo kwa
nini benki hiyo inatoza kiwango kikubwa cha riba kwa wanawake katika
mikopo, wakati inapewa fedha na Serikali kwa ajili ya kusaidia kundi
hilo.
Pia waziri huyo ametangaza kiama kwa
wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya wasiotenga asilimia tano ya
bajeti yao kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya wanawake, kuwa kuanzia
sasa, watakaoshindwa kutimiza agizo hilo,
watatumbuliwa majipu. Alisema
hayo jana kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani,
jijini Dar es Salaam.Alisema
alishitushwa na taarifa aliyopatiwa juzi katika sherehe za kukabidhi
mikopo kwa wanawake zilizofanywa na Benki ya Posta Tanzania (TPB), baada
ya kubaini kuwa benki hiyo ya wanawake inatoza kiasi kikubwa cha riba
katika mikopo yake.
“Nilisikitika sana kusikia eti TPB
inatoza vikundi vya akina mama riba ya asilimia 11 wakati benki ya
wanawake inatoza riba ya zaidi ya asilimia 19. Hili siwezi kulikubali
hivi inaingia akilini kweli wanawake kushangilia benki nyingine wakati
ipo benki ya wanawake kwa ajili yao, tena iliyoanzishwa kwa ruzuku ya
Serikali? Alihoji.
Alimtaka Mkurugenzi wa benki hiyo,
Margareth Chacha (aliyekuwepo kwenye maadhimisho hayo), kumpatia maelezo
ndani ya siku tatu kwa nini benki hiyo inatoza kiwango hicho kikubwa
cha riba. “Nataka mnieleze kwa nini benki hii si rafiki kwa wanawake
wakati inapewa fedha na Serikali.”
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WAZIRI UMMY‘AMKOROMEA MKURUGENZI BENKI YA WANAWAKE
Reviewed by Newspointtz
on
07:23:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment