Serekali imemuagiza afisa madini kanda
ya kati kuifutia leseni kampuni ya madini ya Meek Maine CO.LTD ya jijini
Dar-es-Salaam kwa kushindwa kuanza uchimbaji katika vitalu vitatu
kwenye machimbo ya dhahabu ya Sekenke wilayani Iramba kwa zaidi ya miaka
sita, na kusababisha wachimbaji wadogo kushindwa kujipatia kipato
kutokana na wao kushindwa kufanya kazi kati maeneo hayo.
Naibu
waziri wa Nishati na Madini Daktari Medardi Kalemani amesema hayo
katika kijiji cha mgongo wilayani Iramba kufuatia kampuni inayo
julikana ya Meek Maine CO LTD kushindwa kuchimba madini ya dhahabu
licha ya kupewa leseni hiyo miaka mingi.
Katika hatua nyingine naibu waziri
amesema kampuni hiyo pamoja na kupata msamaha wa zaidi ya shilingi
milioni ishirini na sita wa kuingiza vifaa nchini vya uchimbaji lakini
havijafanya kazi, jambo ambalo ni uharibifu wa fedha za serekali kwa
sababu zingeweza kufanya kazi zingine.
Awali mkurugenzi wa kampuni ya Meek
Maine ambayo aimepewa kibali cha uchimbaji wa madini Bwana Ibrahim Mtulo
pamoja na kukiri kuwa bado hawaja anza uchimbaji licha ya kuwa na
leseni, amemwambia naibu waziri kuwa wao wanajipanga na wataanza
uzalishaji ndani ya miezi sita ijayo.
Kwa upande wao wachimbaji wadogo ambao
wameonekana kuwa na furaha baada ya naibu waziri kufika eneo ambalo
mwekezeji hajalifanyia kazi ,wamesema licha wao sasa kusingiziwa kuwa
wamelipwa fidia katika mgodi huo ,lakini wamefanya juhudi za kupata
haki yao mpaka walipo amua kwenda dodoma kuonana na naibu waziri.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WACHIMBAJI MADINI KUNYANG'ANYWA LECENI IRAMBA
Reviewed by Newspointtz
on
07:55:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment