KILOMBERO
Mtu mmoja wilayani kilombero amefikishwa mahakamani kwa
tuhuma ya kukutwa na meno mawili ya kiboko.
Taarfa imefafana kuwa mnamo february 24 mwaka huu
majira ya saa 9 usiku mtu aliyejulikana kwa jina la Juma Siagi mkazi wa Mji
mwema kamwene jimbo la Mlimba amekamatwa na meno mawili ya kiboko mali
ya Serikali yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki nne arobaini na tano
Kwa upande wa mshtakiwa bwana Siagi amekana kuhusika
na tuhuma hiyo baada ya kufikishwa mahakamani kusomewa shitaka hilo na mwendesha
mashtaka bwana Devidi kinjage mbele ya hakimi mkazi Binge Mashabala.
Mtuhumiwa yupo nje kwadhamana mbaka itakapo sikilizwa tena
march 28 mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment