Mbunge wa Meatu amemuomba waziri mkuu
kuchukua hatua stahiki dhidi ya mwekezaji anayejihusisha na shughuli za
uwindaji wilayani Meatu mkoani Simiyu anayedaiwa kuwadhalilisha
wananchi.
Aidha mbunge huyo ameiomba serikali
kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa mipaka baina ya pori la akiba la Maswa na
vijiji vinavyopakana na hifadhi hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi
katika mkutano wa hadhara, Mbunge huyo wa Meatu amedai kuwa kero kubwa
inahusisha kampuni binafsi ya mwekezaji ambayo waannchi wamekuwa
wakiilalamikia kwa madai ya kuwatesa kwa vipigo hali ambayo amesema
haipaswi kuendelea
Akijibu
malalamiko hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali haiwezi
kumuona mwekezaji akifanya vitendo viovu pasipo kuheshimu sheria za nchi
ambapo amemuagiza mkuu wa mkoa wa Simiyu Elaston Mbwilo kukutana na
mwekezaji huyo na kupitia mikataba yote na taarifa itolewe kwa waziri
mkuu ifikapo Machi 11 na kwamba iwapo atakuwa amekiuka baadhi ya
vipengele serikali itachukua hatua stahiki.
Wakati huo huo waziri mkuu Kassimu
Majaliwa amesitisha ziara wilayani maswa kufuatia kifo cha ghafla cha
Mkurugenzi wa halmashauri ya Maswa Trasiasi Kagenzi aliyefariki dunia
jana katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikofikishwa kwa
matibabu baada ya kuanguka ghafla juzi wakati akiwa kwenye mazoezi.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WAZIRI MKUU AAGIZA ‘KUTUMBULIWA’ KWA MWEKEZAJI SIMIYU
Reviewed by Newspointtz
on
07:40:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment