WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
tatizo la rushwa barani Afrika linasababisha upotevu wa dola za Marekani
bilioni 150 kila mwaka.
Akihutubia wajumbe wa mkutano wa tano
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) linaloendesha vikao vyake jijini Dar
es Salaam, Waziri Mkuu ambaye alimwakilisha Rais Dk. John Pombe
Magufuli, amesema rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma
maendeleo ya Afrika.
Amefafanua kuwa rushwa yaweza kutolewa
kwa njia kuhonga fedha, kupata fedha kwa kula njama, kujipatia fedha kwa
njia za udanganyifu, ama kwa njia za vitisho.
Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa
Afrika (AU), rushwa na urasimu vimeainishwa kuwa ni vikwazo vikubwa
vinavyochangia kuchelewesha ufanyaji wa biashara kwenye mipaka ya nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki, licha ya kwamba sekta binafsi
inachukuliwa kama injini ya maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Hata hivyo Waziri Mkuu ametumia fursa
hiyo kuipongeza jumuiya ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kwa
kuandaa kanuni za kiutendaji ambazo zimelenga kuhamasisha uadilifu
kwenye ufanyaji wa biashara unaozingatia haki za binadamu, sheria za
kazi, utunzaji mazingira na vita dhidi ya rushwa.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
WAZIRI MKUU AFICHUA HAYA MAPYA JUU YA RUSHWA AFRIKA
Reviewed by Newspointtz
on
07:47:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment