NEWSPOINTTZ.BLOGSPOT.COM

WAZIRI WA KILIMO ATOA AGIZO VOCHA ZA PEMBEJEO

 

 

Serikali ya Tanzania imewaagiza mawakala wa Pembejeo za kilimo nchini kuhakikisha kuwa wanawafikishia wakulima vocha za pembejeo za kilimo kwa wakati ili waweze kuzalisha chakula kwa wingi na nchi kuwa na uhakika wa chakula.

Agizo hilo limetolewa na waziri wa kilimo, uvuvi na mifugo Mwigulu Nchemba kufuatia malalamiko ya wakulima wilayani Rungwe mkoani Mbeya ya kucheleweshewa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea hali inayopelekea kuzalisha chakula kidogo tofauti na matarajio

.Kumekuwepo na malalamiko kutoka kwa wakulima dhidi ya mawakala wa Pembejeo za kilimo mkoani Mbeya ya kupewa Vocha za Mbejeo baada ya msimu kuanza hali inayopekea wakulima hao kuhisi watendaji na mawakala wana nia ya kuhodhi pembejeo hizo.

Waziri Nchemba amesema wakulima wanahitaji kuzalisha kisasa kwa kuzalisha chakula kwa wingi kwa kutumia mashamba madogo na kuwa Serikali itahakikisha inawapatia mbegu bora ili kutimiza adhma hiyo.

 

 

chanzo>mtembezi 

 

Share on Google Plus

News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook , Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.

0 comments:

Post a Comment