Paul Simwela Ofisa Tarafa wa Mkunya |
MTWARA Na; Sigfrid Bina
Maafisa
Watendaji wa Serikali wa kata na vijiji Wilayani Newala Mkoani Mtwara
wametakiwa kutojichulia maamuzi binafsi katika matumizi ya mali za umma
kwani kufanya hivyo ni kinyume cha utaratibu wa utendaji.
Hayo
yamebainisha jana tarehe 6 April 2016, na Ofisa Tarafa ya Mkunya Bwana
Paul Simwela ofisini kwake mjini Newala wakati anatolea ufafanuzi juu ya
hatua zilizochukuliwa kwa Ofisa Mtendaji wa kijiji cha Mnalale Bw.
Awadhi Rashid Hulewa baada ya kuchukuwa madawati shule bila ruhusa na
kutengeneza meza za ofisi ya kijiji ambazo nazo aliziuza.
Simwela
amesema kitendo hicho hakikubaliki kwa kiongozi wa umma kuwa kiongozi
wa kutenda mauovu kwa kuhujumu maendeleo ya wananchi wanaowatumikia na
kurudisha nyuma juhudi za serikali za kupambana na umasikini hasa
ukizingatia sekta hiyo ya elimu inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwamo
upungufu wa madawati.
Katika
hatua ya kukomesha tabia hiyo, mtendaji huyo amevuliwa madaraka,
ameamriwa kurejesha madawati aliyoyachukua ndani ya mwezi huu wa nne,
vinginevyo atafikishwa mahakamani, hatua nyingine ni pamoja na Ofisa
Mtendaji wa Kata ya Mcholi moja kutakiwa ndani ya siku 5 ahakikishe
amechagua mtendaji mwingine kutoka ndani ya wajumbe 25 wa halmashauri ya
kijiji.
Ofisa
Mtendaji huyo amekiri kuchukua madawati hayo mali ya shule ya Msingi
Mnalale Kata ya Mcholi 1 wilayani Newala na kwenda kubadilisha matumizi
kwa kutengeneza Meza mbili za ofisi ya kijiji ambazo pia aliziuza kwa
Bw. Nuru Maneno na Bw. Kabunda wakazi wa Mcholi Godauni kwa Tsh,
25,000/= kwa meza zote.
Hulewa
amesema alichukuwa mbao hizo na kuahidi kuzirejesha baadae hivyo japo
na kukiri kuchukua bila taarifa lakini lengo lake ni kuzirejesha baada
ya ofisi kupata fedha ya kununulia thamani hizo.
Fundi
seremala aliyefanya kazi hiyo Mustapha Hassan amesema meza hizo
zilitumia mbao za madawati manne na zingine zilibaki, ambapo Mwalimu
mkuu wa Shule hiyo Alfani Mussa Mohamed amesema madawati yaliyopotea ni
10 na shule yake ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa madawati 25 hivyo
kuongeza ukubwa wa tatizo.
Aidha
pia Mwalimu mkuu huyo amebainisha kuwa wizi huo uliotokea wakati wa
likizo ya mwezi December ambapo baada ya kufungua shule ndipo walibaini
tatizo hilo ikiwa pamoja na upotevu wa Betri 2 za Solar shuleni hapo
msaada wa 21st Century, Kitanda kimoja na magodoro 2 huku wizi huo wa
Kitanda na magodoro ukihusishwa na mtendaji huyo ambapo kesi yake ipo
kituo cha Polisi Newala.
0 comments:
Post a Comment