POLISI
mkoani Katavi inamshikilia Pisikitu Michael (39) kwa tuhuma za kumuua
mwenzake wakati wakigombea pombe za viroba, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Katavi, Damas Nyanda alisema.Michael
anatuhumiwa kumpiga Shukuru Korongo (32) na kumsababishia maumivu na
baadaye marehemu huyo kufariki dunia, wakati wakigombea viroba kwenye
sherehe ya jirani yao.
Kaimu Kamanda Nyanda alisema mauaji
hayo ni matokeo ya kupigana kulikoanza baada ya mmoja wao kufyonza kwa
haraka viroba vyake na kutaka kuchukua vya mwenzake.
Alisema tukio hilo lilitokea Jumatano
saa 5.00 usiku wakati wakiwa kwenye sherehe ya mtoto mchanga aliyekuwa
anatimiza siku 40 tangu kuzaliwa.
Alisema wakiwa wanafurahia viroba
hivyo, Michael aliwahi kumaliza vyake na kumuomba rafiki yake amgawie
kwa kuwa Korongo alikuwa anakunywa polepole.
Hata hivyo mwenzake huyo alikataa, alisema Nyanda.
Baada ya kukataliwa, alimnyang’anya huku Korongo akikataa kumpa akieleza kuwa wote walipewa viroba vinne kila mmoja.
Marehemu alimtaka Michael aondoke akalale, kama amemaliza viroba vyake “na awaachie wenye pombe zao waendelee na sherehe.”
Kaimu Kamanda alisema baada ya kuvutana walianza kupigana hadi ikiwalazimu watu kuingilia kati na kuwaamulia.
Baada ya muda mfupi Korongo alianza kulalamika anasikia maumivu makali
tumboni, alisema Nyanda, hali iliyosababisha arudi nyumbani kulala na
kuacha watu wakiendelea na sherehe hizo usiku huo.
Ilipofika asubuhi, Kaimu Kamanda
alisema, mama yake Korongo alikwenda kumuona mwanae lakini alipogonga
mlango huku akimwita hakupata jibu kutoka ndani.
Mama huyo aliamua kuusukuma mlango kwa
nguvu na ulipofunguka aliingia ndani na kukuta mtoto wake
amekwishafariki dunia akiwa kitandani hapo, alisema Kaimu Kamanda huyo.
Mama huyo alikwenda kwa Mwenyekiti wa
Serikali ya mtaa huo kutoa taarifa, na baada ya kuzipokea Mwenyekiti
huyo Margaret Kitunguru alikwenda polisi kuripoti, alisema Nyanda.
Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Katavi Nyanda alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi wakati upelelezi ukiendelea.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Amuua mwenzake kisa pombe aina ya VIROBA
Reviewed by Newspointtz
on
07:38:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment