Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu amempa wiki mbili Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, awe amempatia ripoti
inayohusu kuwezeshwa kwa wanawake wanaoponda kokoto wilayani humo.
Waziri
Ummy ametoa maagizo hayo wakati alipofika halmashauri hiyo kukagua
ujenzi wa Kituo cha Afya kilichopo Kata ya Bugarama kinachojengwa na
kampuni ya mgodi wa ACACIA iliopo Bulyahulu na kuwakuta wanawake mbele
ya majengo hayo wakiponda kokoto kwa kutumia vifaa duni na kwa mkono
Waziri Ummy alisema hivi sasa kuna
vitendea kazi vya kisasa na vya bei rahisi ambayo vitawasaidia wanawake
hao kuwarahisishia kazi hiyo na kuacha kushinda kwa saa kumi wakiponda
mawe hayo ili kupata kokoto.
Alisema haiwezekani wanawake
wanaojishughulisha na shughuli ndogondogo wakaachwa pasipo kusaidiwa
kwani wanawake wengi ndio wanaosaidia familia.
Aidha, Mhe. Ummy alitoa wito wa
kuhamasishwa wanawake wengine katika Kata zote kujiunga kwenye vikundi
hususan wale wanaojituma na kujitoa kwa biashara ndogondogo
Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo
Dkt. Hamad Nyembea alisema kampuni hiyo ya ACACIA ilianza ujenzi wa
Kituo cha Afya Julai, 2014 na hadi kukamilika ujenzi huo utagharimu
zaidi ya shilingi bilioni 1.7, na ujenzi wa Zahanati ya Bulyahulu
utagharimu zaidi ya shilingi milioni 300.
News Point inakusogezea habari kubwa za kila siku kutoka kila kona ya dunia. Ungana nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagaram ili uwe wa kwanza kupata habari.
RELATED POSTS
Waponda kokoto wasaidiwe-WAZIRI UMMY
Reviewed by Newspointtz
on
07:40:00
Rating: 5
0 comments:
Post a Comment