Mchezo huo ambao ulikuwa muhimu kw apande zote kwa kuwa Arsenal ilikuwa ikihitaji pointi 3 ili irejeshe matumaini ya kupigania ubingwa, huku wapinzani wao wakihitaji pointi 3 kukwepa mwelekeo wa kushuka daraja, ilikuwa kali lakini ni Arsenal ndiyo waliotawala mchezo huo muda mwingi.
Arsenal ilianza kupata bao lake kupitia kwa Alexis Sanchez katika dakika ya 45 akiunganisha mpira kwa kichwa baada ya kupigiwa pasi kutoka kwa Danny Welbeck.
Baada ya hapo Arsenal ilishindwa kupata bao licha ya kutengeneza nafasi kadhaa.
Kuingia kwa Emmanuel Adebayor ambayeni straika wa zamani wa Arsenal kuliamsha shangwe fulani kwa mashabiki wa timu yake ya Crystal Palace huku wale wa Arsenal wakimzomea. Adebayor aliingia katika dakika ya 64 akichukua nafasi ya Connor Wickham.
Adebayor alitisaidia timu yake hiyo kwa kutoa pasi ya bao kwa Bolasie na kuifanya nafasi ya Arsenal kuelekea kwenye ubingwa kuwa ngumu.
0 comments:
Post a Comment