Waziri
wa habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo amewataka makatibu tawala wa mikoa
na maafisa tawala wa wilaya kusimamia na kuimarisha vyama vya michezo
katika maeneo yao.
Waziri
Nape ameyasema hayo akiwa katika ziara ya kikazi katika mikoa ya Tabora
na Singida ikiwa na nia yakutembelea maeneo yanayohusu sekta za
wizara,kupokea taarifa ya mkoa na kutoa vitendea kazi kwa maafisa habari
na mawasiliano wa mikoa husika.
“Tunalo
tatizo la kuangalia vyama vya michezo katika ngazi ya Taifa peke
yake,matokeo yake mikoani huku hali inakuwa mbaya na vyama vya michezo
hivi viangaliwe kwa upana wake na sio mpira wa miguu tu,” alisema
Waziri Nape.
Aidha
waziri huyo mwenye dhamana ya michezo alisema kuwa mpira wa miguu
umeingiliwa na wapiga dili kwani suala la rushwa kwa sasa limekithiri
sana na hasa upangaji wa matokeo na hili linatokea hasa kwa kuwa vyama
vya michezo ni legelege na hivyo wanatengenezwa watu wanajiita viongozi
wa michezo kwenye mikoa na wilaya lakini ukweli wanatengenezwa wapiga
kura wa kwenda kuwapigia kura wakubwa na wala hawana mpango na vyama vya
michezo kwenye mikoa na wilaya zetu.
Pia
waziri uyo amewaagiza makatibu tawala wa mikoa na maafisa tawala wa
wilaya kuhakikisha wanavijua na pia kukutana na vyama vya michezo vya
mikoa na wilaya zao ili kuhakikisha chaguzi zinafanyika kwani wao ndo
walezi na wenyeviti wa kamati za maendeleo ya michezo za wilaya na
mikoa na ambae hatofanya hivyo atataftiwa kazi nyingine na kubainisha
kuwa utawekwa utaratibu wa kuwakumbusha kwa maneno na kwa maandishi kwa
namna hii tutafika mbali katika michezo nchini.
0 comments:
Post a Comment