Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi
Andrea Kigwangalla, ametembelea Hospitali ya Taifa ya Kifua Kikuu
Kibong’oto eneo la Sanya Juu Wilani Siha Mkoani Kilimanjaro.
Dkt.
Kigwangalla katika Hospitali hiyo, alipata kitembelea maeneo mbalimbali
ikiwemo wodi za wagonjwa wa Kifua Kikuu (TB) ya kawaida na ile kali
ambapo pia aliweza kutembelea eneo la kituo cha utafiti cha magonjwa
hayo pamoja na Maabara.
Kihistoria
Hospitali hiyo ya Kibong’oto ilifunguliwa rasmi 29 Oktoba mwaka 1952 na
Lady Twining, baada ya miaka saba ya vita ya pili ya dunia chiniya
utawala wa Muingereza na imekuwa ikitoa huduma hiyo ya magonjwa ya
kuambukiza hususani Kifua Kikuu.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali hiyo, Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Kuambukiza, Dkt Riziki Kisonga amemwelezea Naibu Waziri
changamoto mbalimbali ikiwemo suala la nyumba za watumishi na mambo
mengine ikiwemo suala la bajeti ya vifaa tiba.
0 comments:
Post a Comment