Siku
moja baada ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Anne Kilango
kuvuliwa uongozi kwa kutosema ukweli, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Hawa
Ng’humbi ameiruka taarifa ya kutokuwapo kwa watumishi hewa, ambayo
amesema ilimshtua alipoiona kwenye televisheni.
Mkoa
wa Shinyanga unaundwa na wilaya tatu ambazo ni Shinyanga, Kishapu na
Kahama zinazoundwa na halmashauri sita ambazo ni Kishapu, Manispaa ya
Shinyanga, Mji wa Kahama, Ushetu, Msalala na Shinyanga Vijijini.
Rais
John Magufuli juzi alitengua uteuzi wa Kilango, ikiwa ni siku 30 tangu
alipotangaza kumteua kwa maelezo kuwa alitoa taarifa isiyo ya kweli kuwa
Shinyanga hakuna watumishi hewa kabla ya kujiridhisha.
Pamoja
na Kilango, Rais Magufuli pia alitengua uteuzi wa Katibu Tawala wa
Shinyanga, Abdul Dachi, kwa sababu hiyo ya kutoa taarifa za uongo.
Dk
Magufuli alichukua uamuzi huo baada ya kutuma timu mkoani Shinyanga
kufanya uhakiki na kubaini kuwa kulikuwa na watumishi hewa 45 katika
wilaya moja ya Shinyanga kabla ya kwenda wilaya nyingine za Kahama na
Kishapu.
Akizungumzia
sakata hilo jana baada ya uamuzi wa Dk Magufuli, Ng’humbi alisema
taarifa za kukosekana watumishi hewa kwenye wilaya yake alizisikia
kwenye taarifa ya habari ya televisheni Machi 30 na zilimshtua.
“Binafsi
nilishtuka sana nilipoona ikitangazwa kuwa mkoa mzima wa Shinyanga,
hakuna mfanyakazi hewa wakati mimi sikuwa hata nimeona taarifa kutoka
wilayani kwangu iliyoandaliwa na uongozi wa halmashauri,” alisema Ng’humbi.
“Nilijiuliza
taarifa imefikaje kwa mkuu wa mkoa bila kupitia kwangu? Kusema kweli
nilianza kuifanyia kazi taarifa hiyo na ninatarajia ifikapo Ijumaa
nitakamilisha kazi hiyo.”
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu, Alphonce Gagambobyaki alisema hadi sasa ofisi yake haijafahamu
nani aliyempa mkuu wa mkoa taarifa ya ukaguzi wa wafanyakazi hewa kwa
sababu taarifa aliyonayo mezani haijasainiwa.
“Kuna
tatizo la ofisi hii kukaimiwa na zaidi ya watu wanne tangu aliyekuwa
Mkurugenzi Mtendaji, Dalikunda Kimulika alipostaafu Februari. Ni vigumu
kujua nani alihusika nayo bila kuona saini,” alisema Bagambobyaki.
Alisema taarifa hiyo inaonekana haikusainiwa kutokana na hofu baada ya watumishi waliobainika kutokuwapo kwenye vituo vyao vya kazi karibu wote kuonekana kuwa na ruhusa maalumu.
Alisema taarifa hiyo inaonekana haikusainiwa kutokana na hofu baada ya watumishi waliobainika kutokuwapo kwenye vituo vyao vya kazi karibu wote kuonekana kuwa na ruhusa maalumu.
“Wakati
bado tunajiridhisha kujua ni ruhusa ya aina gani na hawa watumishi wako
wapi, ndipo taarifa ilipotangazwa kwamba mkoa hauna watumishi hewa,” alisema.
Hata hivyo, alisema anaamini taarifa sahihi itajulikana baada ya timu maalumu iliyotoka Tamisemi kukamilisha uhakiki wilayani humo jana.
Hata hivyo, alisema anaamini taarifa sahihi itajulikana baada ya timu maalumu iliyotoka Tamisemi kukamilisha uhakiki wilayani humo jana.
“Timu
ile ya Tamisemi imekwenda mbele zaidi katika uhakiki wake kwa kukagua
mtumishi mmoja mmoja hadi vijijini na imekamilisha kazi yake jana,” alisema Bagambobyaki.
Kuhusu iwapo aliyekuwa mkuu wa mkoa alitumia taarifa zao au la? kaimu mkurugenzi huyo alisema: “Iwapo RC alitumia taarifa zetu au la, hilo siwezi kulisemea kwa sasa.”
Kuhusu iwapo aliyekuwa mkuu wa mkoa alitumia taarifa zao au la? kaimu mkurugenzi huyo alisema: “Iwapo RC alitumia taarifa zetu au la, hilo siwezi kulisemea kwa sasa.”
Kilango
ambaye juzi alisema hakuwa amepata taarifa hivyo asingeweza kuzungumzia
kutenguliwa kwake, jana alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kabisa na
Dachi akaeleza kuwa ameupokea uamuzi huo kwa kuwa Rais ndiye mteule wake.
Taarifa
ya kutenguliwa kwa watumishi hao wa umma sasa imekuwa kaa la moto kwa
wakuu wa wilaya makatibu tawala wao, na wakurugenzi watendaji wa
halmashauri za mkoa huo.
Alipoulizwa
kuhusu taarifa hizo za watumishi hewa, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga,
Josephine Matiro alisema hawezi kuzungumzia lolote.
“Sisemi lolote na wala sizungumziii mkoa,” alisema na kukata simu ambayo haikupokewa tena.
Kama ilivyokuwa kwa mkuu wake wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna aligoma kuzungumzia uwezekano wa halmashauri yake kutoa taarifa zilizompotosha Kilango.
Kama ilivyokuwa kwa mkuu wake wa wilaya, Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Shinyanga, Lewis Kalinjuna aligoma kuzungumzia uwezekano wa halmashauri yake kutoa taarifa zilizompotosha Kilango.
“Sitaki kulizungumzia hilo, nawaachia wanaolijua walizungumzie,” alisema Kalinjuna.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Vita Kawawa alikata simu yake mara kadhaa alipopigiwa na baadaye kutuma ujumbe mfupi wa maneno akisema yuko kwenye kikao na kuelekeza atumiwe ujumbe ambao hata alipotumiwa hakujibu.

0 comments:
Post a Comment