Michezo ya robo fainali ya Ligi ya Vilabu barani Ulaya (UEFA Europe League) imechezwa usiku wa kuamkia Ijumaa kwa michezo minne huku mchezo mkubwa uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka duniani ni mchezo wa Dortmund waliokuwa wakiikaribisha Liverpool.

Mchezo huo umevuta hisia za wengi kutokana na kocha wa zamani wa Dortmund, Jurgen Klopp kurejea katika uwanja wa Dortmund, Signal Iduna Park akiongoza timu nyingine ya Liverpool.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli moja kwa moja, Liverpool ikiwa ya kwanza kupata goli kupitia Divick Origi dakika ya 36 na baadae Mats Hummels akaisawazishia Dortmund dakika ya 48.

Baada ya mchezo huo wa kwanza, mchezo wa marudiano unataraji kuchezwa Alhamisi ya Aprili, 14 katika uwanja wa nyumbani wa Liverpool, Anfield.

Matokeo ya michezo mingine ni;

Athletic Bilbao 1 – 2 Sevilla

Braga 1 – 2 Shakhtar Donetsk

Villarreal 2 – 1 Sparta Prague