Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye (Pichani)
ameahidi kurudisha heshima ya michezo na pia kuhakikisha ubora wa
viwanja unakuwa wa hali ya juu, akianzia na Uwanja wa Nyamagana wa jiji
la Mwanza.
Aliahidi hilo wakati waziara
yake juzi Mkoani Mwanza alipokuwa anauzungumzia uwanja wa michezo wa
kihistoria wa Nyamagana. Alielezea kushangazwa na kudumaa kwa maendeleo
ya uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kusuasua kwa mradi wa kuwekwa kwa
nyasi bandia.
“Nimeanza
kushughulikia suala la nyasi za Nyamagana tangu nilipoingia madarakani,
shida ninayoina hapa ni kwamba ukarabati mwingine unashindwa kuendelea
kutokana na kutokuwepo kwa nyasi bandia.
“Sasa nyasi bandia
nitalimaliza, mimi nashughulika nalo hilo lipo kwangu lakini haya maeneo
mengine mpango ukoje?” Alihoji akimuuliza Ofisa Michezo wa Jiji la
Mwanza, Mohammed Bitegeko.
Aliendelea kusema: “Hapa pana
uzembe mkubwa ambao unaendelea, kila mtu ukimuuliza maendeleo ya huu
uwanja anazungumza mambo ya nyasi bandia, lakini huu uwanja inaonyesha
una awamu zaidi ya moja za ukarabati.
Hivi kila kitu kimesimamishwa
na nyasi bandia? “Kwenye suala la nyasi bandia nawapongeza Jiji kwa
kutoa fedha zenu. Mchakato ulivurugika juu kwa wakubwa huko kwa sababu
TFF (Shirikisho la Soka Nchini) walipaswa kusimamia hili mapema,”
alisema.
Aliongeza kuwa, TFF walipaswa
kuzungumza na serikali mapema kwani kwa kawaida vifaa vya michezo
haviingizwi bure, bali hulipiwa. Nape amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
John Mongella kushirikiana na Jiji la Mwanza katika ukarabati wa uwanja
huo .
Aidha, Bitegeko alisema Halmashauri ya Jiji imeanza mazungumzo na
TFF kuweza kupata michoro ya majukwaa na maeneo mengine ya ndani ya
uwanja.
Uwanja wa Nyamagana unavyoonekana…
0 comments:
Post a Comment