Jeshi
la Zimamoto linaendelea kuutafuta mwili wa mwanamke mmoja aliyekuwa
ndani ya gari aina ya Hiace ambalo limetumbukia bahari ya Hindi leo
alfajiri mara baada ya kuteleza kutoka kwenye kivuko kilichokuwa
kinaelekea upande wa Kigamboni.
Kwa
mujibu wa msemaji wa jeshi hilo, Briton Monyo, ajali hiyo imetokea
majira ya saa 10 alfajiri na hadi sasa wameweza kuupata mwili dereva wa
gari hilo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 29-30.
Monyo
anasema gari hilo litakuwa limetitia chini kwa eneo ambalo tukio
limetokea lina kina kirefu cha maji, tope jingi na vumbi na huku jeshi
likiwa halina vifaa vifaa kama darubini ya majini.
Hata
hivyo, ndugu wa mwanamke anayetafutwa wanasema jana walitoka Mbeya
kwenye msiba wa ndugu yao na gari walilopanda la magazeti liliwaacha
eneo Feri saa 10 alfajiri wakati huo kivuko kilikuwa kimefika ndipo
walipoingia na kukutana na Hiace na kukubaliana na dereva kuwafikisha
makwao mara baada ya kuvuka ng’ambo ya pili.
Hata
hivyo, mwanamke huyo alikuwa amechoka na kuingia ndani ya Hiace huku
ndugu wengine tisa wakakaa sehemu ya abiria ya kivuko.
“Lakini kabla panton halijaanza kuondoka tulishangaa Hiace ikiserereka na kutumbukia” mmoja wa ndugu hao alisema.
0 comments:
Post a Comment